Alhamisi 20 Novemba 2025 - 23:13
Hivi Ndivyo Utakavyokuwa Mpenzi wa Mungu

Hawza/ Kuwatumikia waja wa Mungu ni miongoni mwa matendo yenye kupendwa sana na Mwenyezi Mungu, na yametajwa pia kuwa ni kafara ya madhambi.

Shirika la Habari la Hawza -  Amīrul-Mu’minīn (a.s.) katika Nahjul-Balāgha, kuhusu ukubwa wa kuondoa huzuni katika uso wa wengine, anasema hivi:

«مِنْ کَفَّارَاتِ الذُّنُوبِ الْعِظَامِ، إِغَاثَةُ الْمَلْهُوفِ وَ التَّنْفِیسُ عَنِ الْمَکْرُوبِ.»

“Miongoni mwa kafara za madhambi makubwa ni kumwokoa mwenye shida na kumpa faraja aliye na dhiki.” (1)

Yaani, miongoni mwa kafara za madhambi makubwa ni kumsaidia aliyekata tamaa au aliyedhulumiwa na kumfariji mtu mwenye huzuni.

Sherehe:
Miongoni mwa maagizo makubwa ya Uislamu ni kuondosha huzuni na dhiki kutoka kwenye uso wa ndugu muumini. Kumsadia mja wa Mwenyezi Mungu na kumuondoshea shida ni jambo lenye athari kubwa mno, kiasi kwamba halilinganishwi na amali nyingine.

Imam Sādiq (a.s.) katika riwaya moja kuhusiana ukubwa wa kumuondoshea huzuni ndugu muumini, anasema:

«إذا بَعَثَ اللّهُ المؤمنَ مِن قَبرِهِ خَرَجَ مَعهُ مِثالٌ یَقدُمُ أمامَهُ، کُلَّما رَأی المؤمنُ هَوْلاً مِن أهوالِ یَومِ القِیامَةِ قالَ لَهُ المِثالُ: لا تَفزَعْ و لا تَحزَنْ ... فیقولُ لَهُ المؤمنُ: ... مَن أنتَ؟ فیقولُ: أنا السُّرورُ الذی کُنتَ أدخَلتَ علی أخیکَ المؤمِنِ.»

“Mwenyezi Mungu anapomfufua muumini kutoka kaburini mwake, hutoka pamoja naye mfano (kiumbe) fulani kinachotangulia mbele yake. Kila mara muumini anapoona vitisho vya vya Siku ya Kiyama, mfano huo humwambia: ‘Usiogope, wala usihuzunike…’ Muumini humwuliza: ‘…Wewe ni nani?’ Naye humjibu: ‘Mimi ni ile furaha uliyoingiza katika moyo wa ndugu yako muumini.’” (2)

kwa hakika jangwa gumu zaidi ambalo mwanadamu atalikabili pasi na kuwepo njia ya kukimbilia ni Uwanja wa Mahshar na Siku ya Kiyama, ambayo imetajwa kama:
“Siku ya maumivu makali,” (3)
“Siku ambayo nyuso zitakunjwa na ya kutisha mno,” (4) na nyinginezo.

Basi kutenda wema na “kuutupa dajla” hapa duniani, kunamletea mtu faraja na furaha kubwa katika Uwanja wa Mahshar na wakati wa hesabu ngumu ya Siku ya Kiyama, furaha ambayo hailinganishwi na furaha nyingine yoyote.

Katika riwaya yenye mazingatio makubwa, Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) amewataja watu kuwa ni ahlu wa ‘iyāl (familia) ya Mwenyezi Mungu, na mtu mwenye kupendwa zaidi na Mwenyezi Mungu ni yule anayewaletea manufaa familia ya Mwenyezi Mungu.

«اَلْخَلْقُ عِیَالُ اَللَّهِ فَأَحَبُّ اَلْخَلْقِ إِلَی اَللَّهِ مَنْ نَفَعَ عِیَالَ اَللَّهِ وَ أَدْخَلَ عَلَی أَهْلِ بَیْتٍ سُرُوراً.»

“Viumbe wote ni familia ya Mwenyezi Mungu; na mpendwa zaidi kwa Mungu ni yule anayewanufaisha familia ya Mungu na akaingiza furaha katika Ahlu bayt wangu.” (5)

Fikiria mtu ambaye, katika wakati wa dhiki au matatizo ya familia yako wakati wewe hukuwepo, lakini yeye akawasaidia watu wako na kuwatatulia matatizo yao. Bila shaka, moyo wako utamuelekea kwa mapenzi, na utajitahidi kurejesha wema alioufanya; kwa sababu alikuja wakati familia yako ilikuwa kwenye dhiki na akaondoa huzuni katika nyuso zao.

Sasa, fikiria jambo hili hili — kwa kuzingatia kauli ya Mtume (s.a.w.w.) — lakini katika uhusiano na Mwenyezi Mungu. Yeye ambaye hazina zote za ghaibu za mbingu na ardhi ziko mikononi mwake.

Mtu ambaye ataondoa huzuni kutoka kwa familia ya Mwenyezi Mungu, thawabu yake itakuwa ipi?…

Rejea:
1. Nahjul-Balāgha, Hekima ya 24.
2. Al-Kāfī, Juzuu 2, uk. 190.


3. «إِنِّی أَخَافُ عَلَیْکُمْ عَذَابَ یَوْمٍ أَلِیمٍ.» هود/ ۲۶. – Hūd/26.

4. «إِنَّا نَخَافُ مِنْ رَبِّنَا یَوْمًا عَبُوسًا قَمْطَرِیرًا.» انسان/ ۱۰. – Insān/10.

5. Al-Kāfī, Juzuu 2, uk. 164.

Imetayarishwa na Kitengo cha Elimu na Utamaduni cha Shirika la Habari la Hawza.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha